Kuhusu Taasisi ya afya ya kimataifa ya Duke

Taasisi ya afya ya kimataifa ya Duke (DGHI) inaunganisha vyuo vyote vilivyoko Duke katika kutatua changamoto za afya duniani. DGHI inatoa elimu na utafiti wenye ubora wa kiwango cha juu ikitumia njia bunifu za kisasa katika kuelimisha kizazi kipya cha viongozi wa maswala ya afya duniani. DGHI inaongozwa na Dkt. Michael H. Merson, na ina zaidi ya wahadhiri hamsini wanaozingatia utafiti na ufunzaji wa taaluma ya maswala ya afya duniani.

Wakufunzi wa DGHI ni wenye ujuzi na ubora wa hali ya juu katika chuo cha Duke. Wanataaluma  wa DGHI wamejitolea kufundisha, kuelekeza, kukuza na kusaida wanafunzi kupata mwelekeo na mitazamo yao wenyewe katika taaluma ya maswala ya afya duniani. Wakufunzi hawa ni wataalamu katika taaluma zao mbali mbali kama vile sera za umma, utabibu, mazingira, uhandisi na mengineyo. Wakufunzi hawa pia wanatoa maarifa thabiti ya kielimu inayojumuisha mitazamo mingi ya kisasa na muhimu kwa kufanya utafiti wa maswala ya afya duniani.

Je, taaluma ya maswala ya afya ya kimataifa ni nini?

Taaluma ya maswala ya afya ya kimataifa ni medani wa masomo, utafiti na mazoezi unaosisitiza umuhimu wa kufanikisha usawa wa kiafya kwa watu wote. Taaluma ya maswala ya afya ya kimataifa inahusisha taaluma mbali mbali ndani na nje ya jinsia ya sayansi ya kiafya, inalenga utunzaji wa afya ya mtu binafsi, inakuzisha ushirikiano wa kitaaluma na inasisitiza maswala tata ya afya za kimataifa na maghaidhi.

Taarifa ya Ruwaza: Kuimarisha usharifu wa kitaaluma ili kukabiliana na changamato za afya duniani za kisasa, siku zijazo  na kufanikisha usawa wa kiafya duniani kote.

Taarifa ya misheni

DGHI inashughulikia kupunguza tofauti za kiafya katika jamii na ulimwenguni. Kwa kutambua kwamba matatizo mengi ya afya duniani hutokana na kukosekana kwa usawa wa kiuchumi, kijamii, kimazingira, kisiasa na huduma za afya, DGHI inakutanisha timu za taaluma mbali mbali kusuluhisha matatizo tata ya afya na kuelimisha kizazi kijacho cha viongozi wa maswala ya afya duniani.

Malengo ya Taasisi

  1. Kuwa kiongozi katika kutoa elimu ya maswala ya afya duniani inayojumuisha taaluma mbali duniani kote
  2. Kuchochea na kufanya utafiti bunifu unaotoa majibu kwa mabadiliko ya kiinikizo cha magonjwa duniani na kushawishi sera.
  3. Kutengeneza mtandao wenye shupaa wa washirika wakimataifa ili kudabilishana maarifa na ujuzi wa maswala ya afya duniani

 

Kuelimisha kizazi kijacho cha viongozi wa taaluma ya maswala ya afya ya kimataifa: Mipango Maalum ya DGHI

Shahada kamili au Shahada ndogo ya Taaluma ya maswala ya afya ya kimataifa

Shahada kamili na ndogo za Taaluma ya maswala ya afya ya kimataifa inawafundisha wanafunzi kukabiliana na changamoto za afya duniani kupitia mitazamo ya taaluma mbalimbali. Imetungwa kujumuishwa na shahada nyingine ya chuo cha Duke na inatolewa kama shahada pacha. Wanafunzi lazima watimize matakwa ya shahada kuu ya Taaluma ya maswala ya afya ya kimataifa pamoja na mahitaji yoyote ya shahada nyingine katika chuo cha Duke. Wanafunzi, pia, wanahitajika kupata elimu ya kimaarifa nje ya darasa kwa muda usiopungua wiki nane katika jamii iliyoathirika kiafya Marekani au kwingineko duniani.

Wanafunzi wanaosoma Shahada kuu ya Taaluma ya maswala ya afya ya kimataifa katika chuo cha Duke wana fursa ya kufumbua kwa kina changamoto za afya duniani huku wakisuluhisha matatizo haya na kuleta mabadiliko duniani. Wanapokamilisha shahada hii, wahitimu watakuwa na ujuzi wanaohitaji kufuata amali mbalimbali na kuendelea na elimu ya ngazi ya juu.

Shahada ya uzamili ya Taaluma ya maswala ya afya ya kimataifa

Shahada ya uzamili Taaluma ya maswala ya afya ya kimataifa ni njia mpya ya kukabiliana na mafunzo ya mbinu za utafiti ya maswala ya afya ya kimataifa na inatayarisha viongozi wa kesho kuweza kuathiri afya duniani. Kanuni kielelezi ya shahada hii ni kwamba majilio yanayounganisha taaluma na sekta mbalimbali ni muhimi kwa afya, kwa vile afya inaathiriwa na vipengele vingi.

Kupitia mtaala nyumbufu, wanafunzi wanakuza ufahamu wa muktadha wa afya, huku wakijifunza kutoka kwa wakufunzi pamoja na wanafunzi wenzao wanaoajilia maswala ya afya duniani kupitia taaluma mbali mbali. Mafunzo haya yanasaidiwa na muda wa maarifa na utafiti katika jamii zilizoathiriwa na afya duni usiopungua wiki kumi hatima yake ikiwa ni tasnifu ya matokeo ya utafiti huu.  

Kozi zinatolewa na wakufunzi kutoka idara mbalimbali katika chuo cha Duke. Kozi zenyewe zinawaruhusu wanafunzi kulenga swala mahsusi kama vile afya ya mazingira au sera za afya. Kozi za hiari zinawaruhusu wanafunzi kujenga ujuzi na maarifa za kibinafsi zinazofaa malengo yao ya amali.

Kwa kawaida, wanafunzi hutimiza masomo haya kwa muda wa mihula mitatu au minne. Wanafunzi hutumia likizo ya msimu wa kiangazi kati ya mwaka wao wa kwanza na wa pili kukamilisha miradi yao ya utafiti katika jamii.

Maombi ya kujiunga kwenye shahada hii yanakubaliwa kila ifikapo Januari. Udhamini unapatikana.

 

Kutafuta sulihisho kwa changamoto za afya duniani

Wakufunzi na wanafunzi wa DGHI wanashiriki katika utafiti wa kisasa unaotatua tofauti za afya duniani. Kupitia ushirikiano katika zaidi ya sehemu hamsini kote duniani, wakufunzi na wanafunzi hawa wanafanya kazi na jamii kutafuta suluhisho bunifu kwa hoja ngumu za afya katika kizazi chetu. Vipaumbele za utafiti vinajumlisha:

  • Saratani
  • Magonjwa ya moyo na ujalifu
  • Magonjwa mapya ya kuambukiza
  • Afya ya mazingira duniani
  • Afya ya akili duniani
  • Afya ya akina mama na watoto
  • Uimarishaji wa mifumo ya afya

duke-campus.jpg